Header

TV1 yaungana na TBC1 Kuwaletea Watanzania Kombe la Dunia 2018 Bure

Kampuni ya Kwese Free Sports Tanzania (KFS) kupitia Televisheni ya TV1 Siku ya Leo imetangaza rasmi kuungana na kituo cha Taifa cha TBC1 kutangaza Michezo ya Kombe la Dunia Bure kwa Wwateja wake huku kukiwa na Wachambuzi waliobobea wakichambua kwa Lugha ya Kiswahili.

Makubaliano hayo baina ya TBC na TV1 Yamefanyika katika Ofisi za TBC zilizopo Mwenge jijini Dar es salaam ambapo Mkurugenzi wa TBC Dkt Ayoub Rioba pamoja na Mkurugenzi wa KFS Joseph Sayi walikuwa ni wawakilishi wa Vituo hivyo viwili.

Kutakuwa na Mechi 32 zikiwemo mechi zote zitakazochezwa na timu za Afrika hatua ya Robo Fainali, Nusu Fainali pamoja na Mechi ya Mwisho ya Fainali zote Watanzania watapata nafasi ya kuzitazama bure kabisa. TBC inapatikana katika Ving’amuzi mbalimbali nchini huku TV1 ikiwa inapatikana Startimes, Continental Pamoja na Ting

Comments

comments

You may also like ...