Header

MAMBO MATATU ALIKIBA AFAA KUZINGATIA KURIDHISHA MASHABIKI!

Alikiba

1. HALI YA SOKO INAVYOBADILIKA

Soko la muziki Africa linazidi kubadilika siku baada ya nyingine, hii inamaanisha msanii yeyote wa muziki inafaa awe makini na tayari kusoma nyakati na jinsi soko linavyo badilika. Alikiba nikati ya wasanii wakubwa Africa kwasasa, ila hajaweza kulikubali hilo nakulitia umakinifu. Kitu ambacho kimeweza kuwaumiza mashabiki wake kwa mda mrefu, nikama Alikiba amekuwa akijifanyia muziki kwa mapenzi yake mwenye ila sikuwaridhisha mashabiki ambao wengi waamechwa wakihaha na kuumia kila wanapotaka kusikia vitu vipya kutoka kwa nguli huyu. Soko la muziki huwalinabadili ila pia huwa laweza kusomeka, hivyo inafaa Alikiba na timu nzima iliyopo nyuma yake waweze kulisoma soko kadri linavyo badilika ili kuwapa mashabiki wake kulingana na jinsi wanavyotarajia. Sauti yake ni nguzo muhimu sana katika sehemu ya muziki wake, ila sauti akiichanganya kwa sawa na muundo wa muziki unaotamba kwa wakati kwenye soko huenda vikamueka pahali pa juu zaidi kuliko alipoa kwasasa.

2. KUTAFUTA SOKO JIPYA

Alikiba inafaa aweze kuanza kufikiria kutafuta masoko mapya kwengine kwa kimombo tunaweza kuita ”a change of musical niche”. Hii ni muhimu sana katika maisha ya mwanamuziki ambaye anaota kuwa na mafanikio makubwa zaidi. Inafaa mwanamuziki asiwe na moyo wa kutosheaka hara kama anahitaji kufika mbali. Na katika njia moja ya kutafuta masoko mapya ni kwa kutumia njia ya kuwashirikisha wasanii wenzake iwe ndani ya nchi yake ama hata nje ya nchi. Kila msanii huwa huwa ana mashabiki wake, hii inamaana wasanii wawili wanapoungana kufanya muziki kwa pamoja basi huleta mashabiki wao pamoja na utakuta project yeyote ile ya muziki inayofanywa na wasanii haswa wakubwa wawili huleta mafanikio ya ajabu mfano ngoma ya Alikiba na kundi la Sauti Sol ”My Conditional Bae” ilivyofanya vyema na kuwavutia wafuasi wa Kenya na Tanzania pamoja.

Alikiba Akibudisha Mashabiki.

3. AKUBALI MUZIKI UNAMASHINDANO

Alikiba kila anapohojiwa na vyombo vya habari amekuwa mwepesi kusema kwamba yeye hafanyi muziki kwa kushindana. Lakini kwakweli muziki wa sasa hata enzi za zama kulikuwa na mashindano. Alikiba anafaa kukubali kuwa yupo kwenye ushindani mkubwa, haswa uwepo wa nguli wa muziki Africa Diamond Platnumz ambaye ana ari na kiu ya kuiteka Africa kimuzi. Alikiba japokuwa anakataa kabisa kushindana na nguli huyu lakini ukweli huu utabaki kuwa pale kwani mashabiki wanazidi kuwashindanisha kwa sana. Dawa ya mashindano haya ni Alikiba kukubali kuwa yupo kwenye mashindano na kuanza mikakati mipya ya kuikabili hali hii ya ushindani na ikiwezekana kuitumia teknolojia mpya kama kigezo cha kuwasha moto wa mafanikio.

Comments

comments

You may also like ...