Header

MSANII BEKA THE BOY KUTOKA KENYA AZIDI KUPIGA HATUA KIMUZIKI!

Beka the Boy akitumbuiza kwenye Mseto East Africa inayoletwa kwa hisani ya Mzazi Willy M Tuva

Msanii kutoka kenya Beka the Boy, amekuwa akipiga hatua za juu zaidi katika kuhakikisha kuwa anapanda katika ngazi za juu kimuziki. Beka ambaye amekuwa akifanya media tour yake ya kwanza kubwa ambayo ilianza katika redio na vitua vya habari vilivyopo Pwani ya Kenya ambako ndiko chimbuko lake, kwasasa yupo mjini Nairobi ambapo shughuli hii ya kufanya interviews na vituo mbalimbali vya habari inaendelea. Katika harakati hizo Beka amekuwa na bahati ya kukutana na wasanii nguli kutoka WCB akiwemo Mboso wakati alipokuwa ameanda kwenye kituo cha redio cha Citizen na Harmonize alipokuwa ameanda kuhojiwa na televisheni ya Citizen kwenye kipindi cha burudani cha 10 over 10.

Hata hivyo Beka ambaye kwasasa anatamba na kibao kipya chake kwa jina ”Nyota”, anasema hana haraka na kufanya collabo na msanii yeyote kwasababu bado anasoma soko la muziki linakaaje. Akihojiwa na jarida la Standard lenye makao makuu jijini Nairobi hivi majuzi alihoji kuwa alipokutana na Hermonize, msanii huyu nyota kutoka WCB alimuuliza kama angependa kujiunga na WCB ila alimujibu kuwa bado anafikiria kufanya uamuzi huo. Sababu kuu pia yeye mwenyewe yupo na na Label yake binafsi kwa jina Double B ambayo inahitaji kukuzwa. Beka kwa sasa amekuwa akionekana akishikana na wanamuziki wakubwa wa nchini Kenya pia na wadau mbalimbali wakubwa wenye ushawishi kwenye game ya muziki si Kenya pekee bali Africa kwa ujumla. Kitu ambacho kimemufanya kujiweka kwenye hatua  za mbele kenye ramani ya muziki Africa Mashariki.

Beka the Boy akiwa na Mbosso kutoka WCB nje ya kitua cha redio Citizen kilichomo nchini Kenya.

Kwa hivi sasa akiongea na Dizzimonline, emesema wakati wowote ule atakuwa anaweza kuliamusha dude. Beka anasema licha ya kibao chake kwa jina Nyota kuwa bado kinapeta vyema kwenye vituo mbalimbali vya habari anahisi nivyema kuachia kazi nyingine. Kazi yenyewe itakuwa inashuka na video yake kwa pamoja kwajina Nimefall, sauti ama audio imerekodiwa na mutayarishi muzoefu wa muziki nchini Kenya producer Totti na video kutengenezwa na staa wa kutayarisha video kali za wanamuziki nguli Africa simwengine ila ni Kevin Bosco.

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...