Header

Lady JayDee ajipanga kwa Ziara ya Afrika

Staa na mkongwe wa muziki Tanzania, Judith Wambura a.k.a Lady JayDee ‘Binti Komando’ ametangaza kinachoonekana kuwa ni ujio wa Ziara yake ya kikazi Afrika.

Akizungumzia utayari wa kujaribu na kufanya mambo makubwa, Binti Komando huyo kupitia ukurasa wake wa instagram ameonesha kuwa anaamini hili la maandalizi ya  Ziara litakuwa kubwa kwake na litakuwa ni lenye kufanikiwa bila kujali changamoto.

“LADY JAYDEE AFRICA TOUR|
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••Nataka kufanya Africa Tour 🗺 |
Siku zote kabla hujaanza kitu unafikiria kukwama na kujiuliza je! Utaweza ?| __________________________________________________________________________________________________________________________
Always kuna sauti mbili ndani yako na moja ndio ya ushindi|💪🏽
Naikataa inayonipa hofu 😧naitaka ile ya ushindi inayoniambia jaribu au fanya utaweza |
Naamka na nina amua kufanya|
Hata kama nitaanguka mara mbili tatu kuinuka kupo, na lazima niendelee|
Siku ya kukata tamaa ndio siku ya kufa ⚰️|
Hata kama ni Tour ya ku Slay tu 💅🏾na kupiga piga picha🤳🏾 nitafanya tu😀” Ameandika Lady JayDee.

Hata hivyo Mkongwe huyu anahesabika kati ya wakongwe wachache Tanzania wenye kolabo nyingi na wasanii wakubwa Afrika ambao ni pamoja na Kidumu kutoka Burundi, Oliver Mtukudzi kutoka Zimbabwe, Salif Keita kutoka Mali, Vanessa Mdee kutoka Tanzania, AliKiba kutoka Tanzania na wengine.

Comments

comments

You may also like ...