Header

Papa Dennis aachia Kolabo akiwa na Ray C, Wasafiri mpaka Afrika Kusini

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya DENNIS MWANGI aka PAPA DENNIS anayefanya kazi chini ya record label ya  MALIZA UMASIKINI  ameachia video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanadada REHEMA CHALAMILA maarufu kama Ray C unaokwenda kwa jina la TORNADO ukimaanisha kimbunga cha mahaba.

Wimbo huu unazungumzia mapenzi ambayo anaependwa kazidiwa na mahaba hadi anahisi mapenzi yake ya nguvu kama kimbunga.

Video ya wimbo huu imetengenezwa nchini Afrika ya Kusini na muongazaji wa video maarufu anae kwenda kwa jina God Father

Mbali wimbo huu PAPA DENNIS Amesha fanya nyimbo na vinara wengi wa muziki wa Africa akiwemo
Mr Flavour (Nigeria) ,Chiddimna  (Nigeria) ,Korode bello (Nigeria) na sasa RAY – C
(Tanzania).

Itazame Video hapa.

 

 

Comments

comments

You may also like ...