Header

Mt Number One atengua kiapo cha Mwaka, Ajiswitch kuongeza idadi ya nyimbo

Msanii wa muziki kutoka nchini Burundi, Etienne Mbarushiman a.k.a Mt Number One amebadilisha ratiba ya ujio wa kazi yake mpya kutokana na mshtuko alioupata kwenye kolabo ya wimbo wake ‘Ukwo Nyene’ aliomshirikisha Masterland.

Akiwa ni mwenye kuonesha furaha ya kupata zaidi ya alichotegemea, Mt ameiambia Dizzim Online kuwa muda wowote kuanzia sasa ataachia kazi nyingine mpya kwakuwa mipango ilikuwa ni kuachia video nne tu za nyimbo kwa mwaka mzima wa 2018 na alisha kamilisha idadi hiyo.

“Nimeamua kubadilisha mipango yangu Coz my fans are now forcing me to do so. I planned differently from what am about to do…Muda wowote from now naaachilia moto mwingine and this project nitaachia was in my plan to be out in the begining of Next Year but Mafans wamenifurahisha vile wamepokea song yangu hii nimefanya na Masterland. This is wow…I must give them what they need then…Mwezi mmoja Burundi inasema sana juu ya hii song…Feedback ya media ni Crazy Boss, Reception is Fire…Am telling u” Amesema Mt.

Hata hivyo wimbo huo ‘Ukwo Nyene’ ni mwezi sasa tangu umetoka rasmi na Mt ameongeza kuwa alichukua hatua ya kuuachia baada ya kuona umechukua muda kwenye store ya nyimbo zake kipindi ambacho alikuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa mashabiki ya kujua ni lini anaachia wimbo mwingine baada ya kufanya vizuri na wimbo wake ‘Spend Money’.

Itazame Video ya wimbo ‘Ukwo Nyene’ wa Mt Number One.

Comments

comments

You may also like ...