Header

NEW VIDEO: FIRE YA DOGO RICHIE

Msanii Dogo Richie

Kila unapotaja wasanii wakali wamuziki ambao wamedumu kwenye muziki kwa mda mrefu nchini Kenya, basi huwezi kuliacha nyuma jina la msanii Dogo Richie. Tanzania Dogo Richie alishawahi kufanya muziki na Sam wa Ukweli awali na bado pia anafanya muziki mkali na kila anapoachia ngoma huwa hit. Dogo Richie ambaye wiki mbili zilizopita aliwaacha mashabiki wengi wakijikuna kichwa, baada ya kutoa madai ya kutatanisha kuhusu ukimya wake kwenye muziki. Akiongea kwa njia ya simu na kituo cha radio cha PiliPili FM kilichoko mjini Mombasa, Richie alifunguka kuwa ukimya wake kwenye muziki ulitokana na kurogwa na msanii mwenza ambaye pia alimupoteza sauti. Japo hakumutaja jina ila alifafanua kuwa katika ngoma yake iliyopita kwa jina muziki majanga, aliwataja wasanii wenza wa kuimba kama Sudi Boy, Nyota Ndogo, Chikuzee, Susumila na wengine, ndio ilikuwa sababu kuu ya masaibu yake. Mmoja kati ya wasanii hawa aliowataja kwenye kibao hicho ambacho kwakweli kilileta utata, alikuwa akimtishia maisha na hatimae alimuendea kwa nguvu za giza na kumpotezea sauti kila mara alipoingia studioni kurekodi muziki ama kupanda jukwaani kutumbuiza kitu ambacho kilimutatiza sana na kusababisha kunyamaza kwakwe kwa mda taarifa aliyoitoa kwa mdomo wake kupitia radio Pilipili kama nilivyoaandika hapo juu.

Dogo Richie (Kulia) akiwa na mtangazaji maarufu Africa Mzazi Willy M Tuva.

Ila anasema baada ya kusumbuka kwa mda, aliwaza na kuamua kumuelezea mama mzazi wakwake na hatimae ilibidi kupelekwa kanisani kupata maombi ya dharura na mwishowe akafunguka. Baada tu ya sauti yake kurudi vyema, Dogo Richie aliingia studio wiki moja iliyopita na kushirikiana na mtayarishi ngulii wa muziki maarufu si Africa Mashariki pekee ila Africa kwa sasa Tedd B. Tedd B ambaye anafahamika vyema kwa kufanya kazi na wasanii wengi wa A list nchini Kenya kama Willy Paul na wengineo wengi, hatimae ameawajibika kuhakikisha ngoma mpya ya Dogo Richie kwa jina ”fire” inatoka kwa hali iliyobora na kuvutia zaidi. Mashabiki wa muziki nchini Kenya wamefurahia kumuona Richy Ree akirudi tena kwa game ya muziki huku kibao chake cha fire kikisambaa kwa hasi kama moto kwenye msitu mkavu wankati wa kiangazi. katika wadau wa muziki ambao wameonyesha kufurahishwa na marejeo ya Dogo Richie ni Mtangazaji maarufu Africa wa kituo cha habari cha Citizen nchini Kenya, Mzazi Willy M Tuva ambaye amepost kipande kidogo cha video kikionyesha wakiwa kwenye gari na Dogo Richie ambaye alikua akiimba kibao chake hiki kipya. Hebu itazame video yenyewe hapa chini.

 

                               

Comments

comments

You may also like ...