Header

Quavo wa Migos na Pharrell Williams waingia Studio, Kolabo yanukia

Rapa, Staa wa muziki na mmoja wa wakali watatu wa kundi la muziki wa Rap la nchini Marekani, Migos, Quavious Keyate Marshall, maarufu kama ‘Quavo’ ameonekana katika dalili za kuandaa kazi ya pamoja na Staa mwenzake, Pharrell Williams.

Kwa mujibu wa mazingira ya wawili hao kupitia ukurasa wa Instagram wa Quavo, iliwekwa picha iliyowaonesha wakiwa studio na picha yao hiyo iliambatana na maelezo mafupi yenye maana ya haraka kuwa wameshirikiana, ‘C H O x P’.

C H O x P

A post shared by QuavoHuncho (@quavohuncho) on

Pharrell Williams naye alitumia picha hiyo kwa kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno yenye ishara ya kuwa wawili hao kushirikiana linajieleza, wala haliihitaji maswali. Aliandika “Dont Ask. ‘You already know”.

Don’t ask. You already know.

A post shared by Pharrell Williams (@pharrell) on

Hata hivyo imehisiwa kuwa Quavo anaweza kuwa ameshirikiana na Pharrell nje ya kundi na kama kutakuwa na uwezekano wa wanakikundi wenzake, TakeOff na OffSet kushiriki pia basi watatokea tu kwenye video kama kutakuwa na mpano hu kama njia ya mojawapo ya wao kutoa mchango kwa mwanakikundi mwenzao huyo.

Kwa sasa Mwanakikundi mwenzao, OffSet anaendelea na matibabu kutokana na kuumia vibaya katika ajali mbaya ya gari iliyotokea wiki iliyopita.

Comments

comments

You may also like ...