Header

Rayvanny awasha rasmi taa za ujio wa Pochi Nene ‘Remix’

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Raymond Shaban Mwakyusa a.k.a Rayvanny amewaweka tayari mashabiki kwa ishara ya ujio rasmi wa Remix ya wimbo wake kwa jina ‘Pochi Nene’ aliomshirikisha S2Kizzy.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameweka picha iliyoandaliwa kimtandao kwa rangi nyeusi iliyoandikwa ‘Pochinene Remix’ na kumalizia kwa viashiria vitatu vya alama za moto bila ameelezo ya ziada hivyo kubaki katika hamu ya wengi kuamini kuwa ni hatua nyingine ya taarifa za ujio rasmi wa kolabo ya Remix ya wimbo wa Pochi Nene.

A post shared by Raymond (@rayvanny) on

Siku kadhaa zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alishaaza kuweka baadhi ya Michano ya wachanaji walioshirikishwa katika Remix ya wimbo huo na kati yao ni pamoja na Rapa Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya na kutoka Tanzania ni wakali wengine ambao ni pamoja na Rosa Ree, Country Boy, Wakorinto na inaaminika kuwa kunauwezekano wakawepo wakali wengine zaidi ya hao.

Comments

comments

You may also like ...