Header

Timmy TDat akwaa kisiki cha Siasa, Video ya wimbo wake yagonga mwamba

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Timothy Owuor a.k.a Timmy Tdat amekutana na kikwazo cha kushindwa kuachia video ya wimbo wake mpya, sababu ikiwa ni mrembo aliye tumika katika video yake iliyotarajiwa kutoka siku za karibuni.

TDat anayefanya vizuri na wimbo wake kwa jina ‘Kitambo’ amezungumza na moja ya kituo cha habari cha nchini humo na kudai kuwa video ya wimbo wake mpya uliokuwa utoke wiki ijayo umekutwa na changamoto ya kukwama kutoka na anayetajwa kuwa ni mwanasiasa na baba mzazi wa mrembo aliyetumika katika video kukataa mwanae asitokee katika video ya msanii huyo.

Swali la kutaka kuwafahamu Baba wa Mrembo na mrembo huyo, Timmy hakuwa tayari kuwataja kwa utambulisho wa kufahamika kwasababu za kiusalama na kudai kuwa Mrembo aliletwa na wakala wa wanamitindo na warembo kwa ajili ya video yake na kuongeza kuwa mpaka anakamilisha video yake hakuwa na taarifa za kuwa mrembo huyo ni mtoto wa mwanasiasa.

Hata hivyo kwa upande mwingine katika hatua ya kujua ni kipi kitafanyika kutokana na chagamoto hiyo ili kuepuka hasara ya muda na kiasi cha fedha kilichotumika, Timmy alisema kuwa hayuko tayari kurudia video kwakuwa ameshatumia gharama za kuwalipa waliohusika kuongoza na kuchukua video hiyo ambayo mpaka sasa haijafahamika lini itatoka rasmi.

Comments

comments

You may also like ...