Header

Otile Brown arudisha kumbukumbu kwenye Changamoto za Maisha

Unaweza ukapitia Changamoto za kila aina katika maisha lakini pale utakapoanza kuonja tamu ya matunda ya miangaiko yako ya kila siku, unaweza ukasimama Mbele ya wenzako na kusema ‘MUNGU KWETU SOTE’. Sasa kuna uwezekano kuwa hilo joto la jiwe amelionja Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Jack Juma Bunda a.k.a Otile Brown.

Staa huyo wa ngoma ya ‘Chaguo la Moyo’, amepika ujio mwingine na mara hii anasikika katika kulizungumzia hilo la kupitia changamoto kisha kuyafikia hatua ya kuweka kati ya wenye mafanikio kwenye wimbo wake mpya ‘Mungu Wetu Sote’.

Miondoko, Midundo na mengine yote yaliyohusika upande wa sauti baada ya Otile Brown kuandika na kurekodi Sauti yake yamekamilishwa na Prodyuza Jegede na Video wa wimbo huo kuongozwa na Director A. Macharia kutoka nchini Kenya.

Itazame Video ya wimbo huo mpya wa Otile ‘Mungu Wetu Sote’.

Comments

comments

You may also like ...