Header

P Unit warudisha majeshi, umoja wao kuandaa Mini Album mwaka huu

Kundi la wasanii wa muziki kutoka nchini Kenya, P Unit wamekanusha taarifa za kuvunjika kwao na kuthibitisha umoja wao kuimarika zaidi, ukweli wa kimya chao na mipango yao kwa mwaka mzima wa 2018.

Wanakikundi hao watatu, Gabu, Frasha na Bon-eyee wakiwa location mjini Mombasa nchini Kenya katika kuandaa video ya wimbo wao mpya unaotegemewa kutoka mwinshoni mwa mwezi ujao, wameiambia Dizzim Online kuwa kimya chao kilisababishwa na majukumu binafsi, kusoma upepo wa tasnia ya muziki na kufanya kila kianchowezekana ili watakapoamua kurudi katika sanaa rasmi wawe na mengi mazuri kwa ajili ya mashabiki wa muziki wao.

Hata hivyo wanakikundi hao wakizungumzia mipango yao kwa mwaka mzima wa 2018, walithibitisha kurudi kwa kasi na kutoa sababu za ziada kuwa wako katika hatua za umalizia wa Mini-Album yao itakayotoka mwaka huu na wimbo ambao unashootiwa Video mjini Mombasa unaokwenda kwa jina ‘Chocha’ utapatikana katika Mini Album hiyo.

Comments

comments

You may also like ...