Header

OTILE BROWN KAFATA NYAYO ZA MSANII BEKA THE BOY KATIKA KUUNDA VIDEO YAKE MPYA?

Msanii Otile Brown

Kama wasemavyo wahenga siku zote chanda chema huvishwa pete, basi naona umefikia mda na wasaa kamili wa msanii Beka the Boy kuvishwa pete. Beka ambaye amekuwa akivuma na kupaa juu sana katika tasnia ya muziki nchini, katika mahojiano na kituo cha runinga cha Citizen TV cha nchini Kenya Beka alishawahi kuwarai sana mashabiki nchini Kenya kumshika mkono maana anauwezo wa kuiwakilisha nchi ya Kenya vilivyo Africa Mashariki na hata zaidi kimuziki. Na kweli maombi yake yamejibika, maana baada ya kutoa kibao chake kinacho vuma kwasasa kwa jina ”Nimefall”, alirudi tena studio kwa mara nyingine tena na mara hii kupitia mikono ya mtaarishi wa video maarufu si Kenya pekee bali Africa kwasasa Dr. Eddy akatoa kibao kingine kwa jina ”Time”.

Msanii Beka the Boy

Video ya Time imekuwa changamoto kwa wasanii wengi nchini Kenya akiwemo msanii Otile Brown ambaye anatamba na ngoma yake mpya kwa jina ”Mungu wetu sote”. Otile Brown baada ya kuiona video ya wimbo wa msanii Beka the Boy ilivyovutia na ustadi wake ikiwemo video queen aliye tumika pale, alivutiwa sana na baada ya hapo aliitafuta video agency inayomiliki hifadhi ya mwanadada huyu mrembo kwa jina Ann Samatha. Ann ambaye ni model aliyeanza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye video mpya ya Beka the Boy ”Time”, amekuwa gumzo kwasasa nchini Kenya hii ni baada ya hatua ambayo nimeigusia hapo juu ya Otile kumutumia tena kwenye video yake mpya ya ”Mungu wetu sote”.

Beka the Boy akiwa na Ann Samatha, video queen aliyetumika kwa wimbo wake (Time) na baadaye katika wimbo wa msanii Otile Brown (Mungu Wetu Sote)

Hatua hii imepokelewa kwa njia mbili na mashabiki wa muziki nchini Kenya, huku mjadala ukiibuka kuwa Otile Brown huenda ameanza kuona hatari ya kufinikwa kimuziki na msanii Beka the Boy ambaye kwasasa amekuwa akikuwa kwa kasi kali kila uchao. Wengi wameitafsiri hatua ya Otile Brown kumutumia Model Ann kwenye video yake kama kuiga ama kuisafiria nyota ya Beka the Boy ambaye kwakweli mwendo wake kimuziki umekuwa ukiangaziwa kuwa hauna kifani na ameonekana kama mpinzani mkuu wa Otile Brown ikilinganishwa wote wanafanya muziki ainamoja wakuimba na pia wote japokuwa wamehamia Nairobi lakini wana chembechembe za asili ya Kipwani yani wote niwazaliwa wa pwani ya Kenya ambako kiswahili na aina ya muziki wao unakaribiana na muziki wa Bongo flava tofauti na wasanii wa Nairobi. Ukumbuke ngoma na video ya Time imetayarishwa na Dr. Eddy, ambaye ndiye aliyemtoa msanii Otile kimuziki kabla ya kukosana na kuvunja mkataba na kila mmoja wao kuenda upande wake kimuziki. Nimekuleta picha zaidi za model huyu hapa chini na video zote mbili alizotumika, hebu zitazame video zote mbili hapa chini ujionee mwenyewe halafu toa maoni yako.

Vera Sidika ambaye ndiye girlfriend wa msanii Otile(Kulia) akiwa location na model wa Time wakati wakishoot video ya Mungu wetu sote.

 

 

Beka the Boy akiwa location na model huyo Ann.

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...