Header

Sean Paul apata msiba wa Baba yake mzazi

Msanii wa muziki wa Reggae na Danso kutoka Jamaika, Sean Paul Francis ‘Sean Paul’ amempoteza Baba yake mzazi, Mzee Garth Henriques aliyefariki siku ya Alhamis baada ya kulazwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili hospitalini kwa kusumbuliwa maradhi ambayo ni sambamba na kupungukiwa na damu.

Sean amethibitisha taarifa hizo kwa masikitiko kupitia kurasa zake za Mitandao ya kijamii ambapo amewashurukuru wote waliohusika kwa namna yoyote kwa kipindi chote cha uuguzaji wa baba yake. Sean alisha bainisha kuwa kumuuguza Baba yake ni moja ya sababu zilizopelekea kutoonekana kwake zaidi kwenye shughuli za muziki kwa miezi iliyopita.

Staa huyo ameomba kujiwekea kiwango cha kujiweka kwenye faragha kwa wakati wa changamoto hii na familia yake.

Comments

comments

You may also like ...