Header

Azam FC yanasa saini ya Donald Ngoma, yaahidi kumpeleka Afrika Kusini kwa Matibabu

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imethibitisha kunasa saini ya Donald Ngoma kwa Mkataba wa Mwaka Mmoja 2018/2019 kuitumikia Klabu hiyo yenye Maskani yake Chamazi.

Mchezaji huyo wa zamani wa FC Platinum ya Zimbabwe pamoja na Yanga amekuwa nje ya Uwanja kwa Takribani Msimu mzima kwa kile kilichokuwa kikiripotiwa na Uongozi wa Yanga kuwa Mchezaji huyo anasumbuliwa na Majeraha.

Uongozi wa Azam FC umesema kuwa baada ya kukamilisha taratibu zote za Usajili watampeleka mchezaji huyo katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona.

Kama Ngoma hatakuwa na Majeraha Makubwa huenda akawa ni miongoni mwa nyota wapya wa timu ya Azam watakaoonekana kwenye Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup) linalotarajia kuanza hivi karibuni huku Klabu hiyo ikiwa ndio Bingwa Mtetezi wa michuano hiyo. Ngoma amekabidhiwa Jezi namba 11iliyokuwa ikitumiwa na mshambuliaji Yahaya Mohammed, aliyerejea Aduana Stars ya nchini kwao Ghana

 

Comments

comments

You may also like ...