Header

Falz avaa viatu vya Childish Gambino nchini Nigeria

Rapa, Muandishi, Muigizaji na Staa wa wimbo ‘ La Fête’ kutoka nchini Nigeria, Folarin Falana, anayejulikana zaidi na jina lake la sanaa ‘Falz’ amezungumzia Nigeria kwa waza la wimbo wa Mchekeshaji, Muimbaji na Muigizaji kutoka Marekani, Childish Gambino ‘This is America’.

Childish Gambino

Rapa Falz amejulikana zaidi kwa kutumia wasifu wake wa sanaa kuzungumzia baadhi ya matatizo na njia kadhaa za utatuzi katika jamii ya nchi yake na mashabiki wa muziki wake wamekutana na wimbo wake mpya kwa jina “This is Nigeria” ikiwa imetumika Beat ya kufanana mapigo ya wimbo halisi wa Chaldish Gambino na video ya wimbo huo ikiongozwa kwa mfano wa ‘This Is America’ chini ya uongozaji wa Iyobosa Geezy Rehoboth ‘Director Prodigeezy.’

Hata hivyo Wimbo huu wa Falz umepata mapokeo makubwa kiasi cha kuzungumziwa zaidi kupitia mitandao ya kijamii na kutoka kwa wingi kwa ripoti mbali mbali za mitandao ya nchini Nigeria juu ya wimbo huo.

Itazame Video ya wimbo ‘This is Nigeria’ wa Falz hapa.

Hii ni video rasmi ya wimbo wa Childish Gambino ‘This Is America’.

Comments

comments

You may also like ...