Header

Sergio Ramos amponda Salah, asema Messi na Ronaldo hawana Mpinzani ndani ya Sayari hii

Beki wa kati wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Hispania Sergio Ramos ametoa neno kwa wale wanaofananishwa na Wachezaji wawili Nyota Lionel Messi pamoja na Mchezaji mwenzie Cristiano Ronaldo kuwa Wachezaji hao wana Uwezo Mkubwa sana kiasi cha kusema si wa Sayari hii.

Nahodha huyo wa Real amezungumza hayo mbele ya Waandishi wa Habari Mjini Kiev nchini Ukraine kuelekea Mchezo wao wa Fainali Usiku wa Leo dhidi ya Liverpool.

“Kwa Mimi kuwafananisha Wachezaji wengine na Ronaldo na Messi si sawa Wawili hawa ni Watu wa Sayari nyingine kabisa, Wachezaji wengi wanakuja na kupotea, Salah amekuwa na Msimu mzuri sana kila Mtu anasifia na huwezi kupingana nao lakini huwezi kumfananisha Ronaldo na Wachezaji wa aina hiyo, kwangu mimi (Salah) amekuwa Bora sana  na amedhihirisha hilo ila anahitaji kufanya hivyo kwa Muda mrefu kama walivyofanya Messi na Ronaldo. Kitu cha Mwisho namtakia Mchana mwema na Mchezo mzuri” Alisema Nahodha huyo ambaye ameiongoza Real Madrid kutwaa Ubingwa wa UEFA mara Mbili Mfululizo.

Real Madrid watakua Uwanjani Usiku wa Leo 21:45 kupambana na Majogoo wa Jiji Liverpool wakitaka kuweka Historia ya kutwaa Ubingwa huo mara Tatu Mfululizo na kufikisha Makombe 13 ya UEFA huku Liverpool wakitaka kuweka Historia ya kutwaa Ubingwa huo mara ya Tano na kuwa ni Timu kutoka Uingereza iliyotwaa Taji hilo mara nyingi zaidi huku Vita nyingine ikiwa ni kati ya Wachezaji Cristiano Ronaldo dhidi ya Lionel Messi

 

Comments

comments

You may also like ...