Header

Kala Jeremiah ahusisha uokovu kati ya sababu za kumchagua Walter Chilambo

Rapa na Staa wa muziki kutoka Tanzania, Kala Jeremiah Masanja a.k.a Kala Jeremiah ametoa sababu za kumshirikisha Walter Chilambo kwenye wimbo wake unaotarajiwa kutoka kwa jina ‘Natabiri’ chini ya utayarishaji wa Prodyuza Zest wa Moja Moja Records.

Kala Jeremiah na Walter Chilambo ni zao la wasanii wa muziki kutoka kwenye mashindano ya muziki Tanzania ‘Bongo Star Search’ na Kala amesema kuwa ameamua kumshirikisha Walter kwakuwa alihitaji kumshirikisha msanii atakaye endana na mudhuhi ya wimbo.

“Sababu ya mimi kumshirikisha Walter Chilambo kwanza ni kwasababu ana uwezo mkubwa wa kuimba, namjua vizuri, namfatilia vizuri lakini pia nilitaka mtu ambaye ataendana na mahudhuhi ya wimbo. Wimbo umekaa kiimani, unaongea vitu flani ambavyo ukisiliza mwenyewe nadhani mtu utaelewa ninachomaanisha” Amesema Kala Jaremiah.

Kala aliongeza kwa kuzungumzia uhusiano wa historia za maisha yao ya muziki kati yake na Chilambo kwa kusema kuwa, inawezekana kolabo ya wimbo huu ikawa ni kazi ya kwanza ya waliowahi kushiriki kwenye mashindano ya Bongo Star Search kushirikiana katika wimbo mmoja.

“Lakini pia tuna historia mimi na Walter Chilambo, sisi wote tumetokea katika shindano la Bongo Star Search kw ahiyo utakuwa ni wimbo wa kwanza wasanii wa Bongo Star Search kushirikiana pamoja hivyo alikuwa na kila sabababu ya kukaa kwenye wimbo na ukisikiliza hii Chorus aliyopiga huyu mtoto nadhani kwa mara ya kwanza watu watamuogopa sana Walter Chilambo, watamuogopa sana sana sana…Kaimba kitu kikubwa sana” Kala Aliongeza.

Kala alishiriki mashindano ya Bongo Star Search(EBSS) ya Mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya nne, na Walter Chilambo aliibuka mshindi wa mashindano hayo msimu msimu mwingine wa ‘EBSS’  wa mwaka 2012.

 

Post ya Ujio wa Kala Jeremiah aliomshirikisha Walter Chilambo ‘Natabiri’

Comments

comments

You may also like ...