Header

“Naweza kufeli Vitu vingine ila sio kwenye Mavazi”:-Hamisa Mobbeto

Mwanamitindo, Mjasirimali na Video Queen maarufu Nchini Tanzania Hamisa Mobetto amekiri kuwa anaweza kushindwa vitu vingi ikiwemo Biashara lakini si kwenye Suala la Ubunifu wa Mavazi.

Hamisa ambaye anamiliki Duka la Nguo za Wanawake na Watoto linaloitwa Mobettostyles ameiambia Dizzimonline kuwa ana ujuzi mkubwa sana katika Masuala ya Mavazi na kamwe hawezi kufeli kwenye Biashara hiyo.

“Watu wameshazoea mabaya tu kwaiyo wakiona kitu kuzuri wanakua hawaamini kama ni Hamisa anaweza kufanya kuna Vitu vingi naweza kufeli kwenye Maisha ila sio Mavazi, ni kitu ambacho nakijua sana ni Fani yangu na ndio kazi yangu” Alisema Mama Dayllan.

Pia Mrembo huyo amezungumzia pia suala ya Watu wanaozusha Maneno kuwa Duka hilo si lake, Hamisa amesema kuwa Mobettostyles ni nguvu yake na alianza kuweka pesa kidogo kidogo tangu akiwa na Ujauzito wa Dayllan.

Comments

comments

You may also like ...