Header

Serena Williams arejea kwa Kishindo, ajifananisha na ‘Queen of Wakanda’

Baada ya kukosekana kwa Takribani Miezi 16 katika Mashindano makubwa Mwanadada Serena Williams arejea kwa kishindo ‘Grand Slam’ baada ya kumuondosha Krystina Pliskova kwa seti 6-4 na 7-6 katika raundi ya kwanza ya Michuano ya French Open.

Serena anashiriki kwa mara ya kwanza Grand slam tangu ajifungue Septemba Mosi Mwaka jana, kwenye Mchezo huo Serena alionekana akiwa amevalia vazi maarufu kama ‘Cutsuit’ ambalo baada ya kuulizwa Serena alisema kuwa ameamua kuvaa vazi hilo coz linamfanya awe comfortable, Jasiri and anajiona kama Wakanda QUEEN akijilinganisha na Wasichana kutoka kwenye Movie ya Black Panther. Serena atakutana na Mwanadada kutoka Australia Ashleigh Barty katika Roundi inayofuata.

 

Comments

comments

You may also like ...