Header

Mourinho aonekana Austria, amuwinda Nyota wa West Ham

Chombo cha Habari cha Sky Sports cha nchini England kimeripoti kuwa Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anawinda Saini ya Mshambuliaji wa Austria anayekipiga katika Klabu ya West Ham, Marco Arnautovic.

Mourinho ameonekana siku ya Jana nchini Austria katika Mchezo wa kirafiki ambao Austria ilishinda Goli 1-0 dhidi ya Urusi huku Arnautovic akitoa Pasi ya Goli hilo.

Arnautovic alijiunga na West Ham Msimu uliopita kwa Mkataba wa Miaka Mitano akitokea klabu ya Stoke City. Mourinho amewahi kumfundisha Arnautovic akiwa kwa Mkopo Inter Millan Mwaka 2009.

Manchester United wanahusishwa pia kuwania saini ya Beki wa FC Porto Diogo Dalot pamoja na Kiungo wa Shaktar Donetsk Fred.

Comments

comments

You may also like ...