Header

Undani wa Bifu la Pusha T na Drake, kumbe lilianza 2012!

Katika Vitu ambavyo si ajabu wala vya kushangaza ni kuona Wasanii wa Hip Hop wakiwa kwenye beef hasa kwa nchi za Wenzetu hususani Marekani tumewai kushuhudia beefs nyingi sana ambazo zinaishia kwenye kutoleana maneno makali sana kwenye nyimbo kwa ufundi sana ambapo kama Shabiki si mfuatiliaji mzuri wa Muziki huwezi kuelewa.

Tuna Mifano mingi iliyo hai kwa Marekani kama unakumbuka Miaka ya 1980 beef kati ya ICE CUBE na Kundi la N.W.A, beef la Mashariki Na Magharibi kati ya 2 pac na the Late Notorious BIG Beef ambalo lilidumu mpaka Miaka ya 1990 ingawa kwa kizazi chetu hichi cha Mwaka 2000 wengi tutakua tunakumbuka sana beef la 50 Cent na Ja rule.

Beefs huama kizazi na kizazi huku zingine zikiibuka tu kama hii ya Drake ambaye ni Moja kati ya Ma rapa wenye uwezo mkali sana dhidi ya rapa wa kizazi hiki cha Social Media Pusha T.

Bifu hilo lilianza Lini???????????

Bifu hii ilianza tangu Mwaka 2012 ambapo Drake na Pusha T wamekuwa wakikosoana. Huenda bifu hili lilikua la chini chini lakini Mashabiki wa muziki wamelifahamu kutoka kwa Pusha T baada ya kulalamika kuwa Drake is Fake hayuko real maana ana Mtu ambaye anamuandikia Nyimbo zake. Pusha alimdis kwenye Wimbo wa Infrared.

The game’s fucked up
Nigga’s beats is bangin’, nigga, ya hooks did it
The lyric pennin’ equal the Trumps winnin’
The bigger question is how the Russians did it
It was written like Nas, but it came from Quentin

Drake akaijibu Diss kwa kumshutumu kuwa Pusha T alikuwa mtumiaji na Msambazaji wa Unga hivyo huenda akawa hayuko sawa. Drake alirudia Diss hiyo kwenye Wimbo wake wa More Life uliotoka Mwaka Jana.

“But really it’s you with all the drug dealer stories

“That’s gotta stop, though

“You made a couple chops and now you think you Chapo.”(Chop ni Drug dealer mdogo Chapo Mkubwa)

Bifu hilo likaendeleaje?

Wiki chache zilizopita Ma rapper hao wamekuwa wakirushiana Maneno kwenye nyimbo na katika Mitandao ya kijamii. Katika Wimbo wa Pusha T wa Daytona uliobeba jina la Album yake mpya iliyotoka Mwaka huu kuna Mstari unaosema:

“How could you ever right these wrongs when you don’t even write your songs?” Haikumchukua Muda hata wa Masaa 24 Siku hiyo hiyo Drake alijibu Diss hiyo kwenye Track yake ya Duppy Freestyle akasema “I’m in shock,” he says at the start of the song. “The nerve, the audacity.” “Man, you might’ve sold to college kids for Nike and Mercedes

“But you act like you sold drugs for Escobar in the 80s.”

Drake akirudia kuhusu Past ya Pusha T. Baada ya hapo wawili hao wamekuwa wakidisiana kila kukicha

 

Bifu limefikia wapi?

Siku ya Jumatano Pusha T aliliamsha Dude baada ya kuachia Wimbo unaoitwa The Story of Adidon ambapo ndani ya Wimbo huo Pusha kamshutumu Drake ametelekeza  mtoto wake anayeitwa Adidon, Mtoto huyo ana Miezi Saba aliezaa na Mwanamke anayeitwa Sophie ambaye ni Muigizaji wa Video za Utupu.

“Adonis is your son, and he deserves more than an Adidas press run, that’s real

“Love that baby, respect that girl. Forget she’s a porn star, let her be your world.”

Cover ya Wimbo huo imetumika picha ya Drake akiwa amepaka rangi nyeusi usoni, Picha iliyopigwa na Mpiga picha David Leyes ambayo baadae iliondolewa kwenye Website ya Mpiga picha huyo kutokana na Watu wengi kuiripoti.

Drake atajibu tena Diss hii? Au atalipa kwenye Album yake ya Scorpion aliyotangaza itatoka Mwezi June? Wacha tusubiri.

 

 

Comments

comments

You may also like ...