Header

Jezi Mpya ya Timu ya Taifa ya Nigeria yageuka ‘Lulu’ Sokoni, Jezi zamalizika ndani ya Dakika chache!

Jezi mpya za Nyumbani za Timu ya Taifa ya Nigeria kwa ajili ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi zimeuzwa zote ndani ya Dakika chache baada ya kuingia Sokoni Alfajiri ya Leo.

Mamia ya Mashabiki wameonekana katika Duka la Nike katika Mitaa ya Oxford Jijini London kununua Uzi huo unaotajwa kuwa ni uzi Mzuri sana miongoni mwa Jezi za Vilabu vingine katika Kombe la Dunia.

Msanii wa Nigeria Wizkid alionekana katika Uzinduzi wa Jezi hizo sambamba na Staa wa Arsenal Alex Iwobi. Awali kampuni iliyotengeneza Jezi hizo ambayo ni Nike ilipokea Oda ya Jezi zaidi ya Milioni Tatu kabla hawajazitoa rasmi. Kwa sasa Jezi hixo hazipatikani mpaka Kampuni ya Nike itakapotoa zingine.

Comments

comments

You may also like ...