Header

Simba yatinga Nusu Fainali Sportspesa Super Cup, Singida kutupa karata yao dhidi ya FC Leopard

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali ya Michuano ya Sportpesa Super Cup baada ya kuibuka na Ushindi wa Penati 3-2 dhidi ya Klabu ya Kariobangi ya nchini Kenya.

Mchezo huo uliamuriwa Matokeo kwa hatua ya Mikwaju ya Penati baada ya Timu hizo mbili kushindwa kufungana ndani ya Dakika 90 huku Shujaa wa Penati ya Mwisho iliyowapeleka Simba nusu fainali akiwa ni Kiungo wake Jonas Jerald Mkude na kuifanya Simba kuondoka na Ushindi wa Penati 3-2.

Mpaka sasa Timu mbili tayari zimetinga hatua ya Nusu fainali, Jana tulishuhudia Timu ya Kakamega wakitinga hatua hiyo baada ya kuifunga Goli 3-1 klabu ya Yanga huku Gor Mahia ya Kenya ikitinga nusu Fainali baada ya kuifunga JKU Magoli 3-0.

Watanzania wanapata Fursa ya kuyatazama Mashindano hayo kupitia King’amuzi cha Star times kupitia kifurushi cha Mambo au kwa malipo ya Siku na akapata Burudani hiyo. Mpaka sasa zimebaki Timu mbili za Tanzania, Singida United pamoja na Wekundu wa Msimbazi Simb SC.

 

Comments

comments

You may also like ...