Header

Infinix HOT 6: SIMU YENYE LADHA YA MZIKI.

Hivi karibuni kampuni ya simu ya Infinix ilifanikiwa kupenya katika soko la simu nchini Tanzania na kuweza kujitambulisha rasmi mwaka huu jijini Dar es Salaam. Infinix Mobility kama inavyotambulika kwa jina ndani ya muda mfupi imeweza kuwaridhisha wa Tanzania kwa uzalishaji wa simu janja kama vile Infinix HOT S3 na Infinix HOT 6 ikiwa simu yao mpya kwa sasa.

Infinix HOT 6 ni simu iliyowavutia wengi kutokana na ubunifu uliotumika kwani kampuni nyingi zimekua zikiwekeza sana kwa upande wa kamera na kusahau vitu kama spika zenye kupiga mziki mzuri, muonekano mzima wa simu na mfumo wa uendeshaji simu nikimaanisha ‘Android’.

Pamoja na kuwa na umbo jembamba la nchi 6.0 HD+ na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9 lakini bado haijazuia simu hiyo kuwa na spika mbili zenye kuchuja na kupiga mziki mzuri hata pasipo na matumizi ya ‘earphone’.

 

Kamera ya ya Infinix HOT 6 ni ‘megapixel’ 13 nyuma na megapixel 8 mbele. Kamera ya nyuma ina ‘aperture’ ya 2.0 na flashi mbili za LED na kamera ya mbele ina ‘aperture’ ya 1.8 na flashi hivi vionjo vyote vinafanya kazi kwa pamoja ikiwa ni kung’aza picha na kupiga picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu.

Infinix HOT 6 ina aina mpya ya ‘security’ yenye ulizi madhubutu ambayo ni ‘face id’.Kupitia ‘face id’ unauwezo wa kunlock simu haraka zaidi kwa kuitazamanisha sambamba na paji la uso. Lakini pia ina ‘fingerprint’ yenye kunlock simu kupitia alama za vidole.

Na pamoja ya kuendeshwa na Android 8.1 na processor ya 1.3ghz quard core vyenye kuipa simu kasi ya kufanya kazi kwa haraka zaidi na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka lakini bado Infinix HOT 6 inabetri lenye ujazo mkubwa wa 4000mAh. Kupitia Infinix HOT 6 unapata uhuru wa kusiliza mziki na kufanya kazi mbalimbali pasipo kipimo.

http://www.infinixmobility.com/tz

Comments

comments

You may also like ...