Header

DStv mambo ni Motoo, Wateja wake kupata Burudani kabambe Kipindi cha Kombe la Dunia

Zikiwa zimesalia siku 3 tu kuelekea katika mashindano ya FIFA Kombe La Dunia 2018 nchini Urussi. DStv watakuwezesha wewe mteja wao kufurahia mechi zote 64 za michuano ya FIFA Kombe la Dunia 2018 LIVE zikiwa kwenye picha ang’avu HD kupitia chaneli zake mpaka 6 maalum zilizoandaliwa kwa ajili ya mchuano hii. Wateja wote wa DStv watafurahia mashindano haya kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu!

DStv pia imekuandalia matangazo ya moja kwa moja ya FIFA Kombe la Dunia 2018 kwa Lugha ya Kiswahili utakaoletwa kwenu na timu yetu mahiri ya wachambuzi Nguli wa soka kutoka hapa nchini akiwamo Oscar Oscar, Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Ibrahim Maestro, Edoku Mwembe, bila kumsahau Ephraim Kibonde watakaokuletea matangazo haya LIVE kutoka Russia.

Kwa kuongezea, DStv imekuleta ofa maalum kwa wateja wake wapya, Sasa wataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure kitakachokuwezesha kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia LIVE mechi zote 64 kupitia chaneli za supersport .

Mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, DStv inataka kuhakikisha kuwa wateja wanaweza kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, laptop na tablet.  Download App yetu ya “DStv Now”, unaweza kutumia hadi vifaa vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako hivyo kuwawezesha wanafamilia kutazama vipindi tofauti  wakiwa sehemu yoyote kwa kutumia vifaa vyao.

Comments

comments

You may also like ...