Header

AKA kufunga Rasmi ukurasa wake wa kufanya album na ‘Touch My Blood’

Rapa na Staa wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Kiernan Jarryd Forbes ‘AKA’ ameonesha kukamilika Rasmi kwa Album yake itakayokwenda kwa jina ‘Touch My Blood’ na taarifa za kuaminika kwa mujibu wa AKA na Uongozi wake ni kuwa hii itakuwa album yake ya tatu na ya mwisho kutoka kwake.

Leo Kwenye Ukurasa wake wa Instagram, AKA ameweka picha ya Mkebe wa CD ulioandaliwa na kupambwa kwa picha rasmi ya cover ya album hiyo na kaundika “Finally … 💽 #TouchMyBlood 💉” ambapo wadau na mashabiki wa muziki wake wataweza kuipata rasmi sokoni Album hiyo siku ya kesho (Juni 15, 2018) kama mambo yataenda kama yalivyopangwa.

Finally … 💽 #TouchMyBlood 💉

A post shared by AKA (@akaworldwide) on

Hata hivyo Album hii inatarajiwa kubeba kiasi kikubwa cha michano na uandishi wa wakali na mastaa wa muziki kutoka nchini Afrika kusini. Pia inatarajiwa kuwa na nyimbo zisizopungua 16 zikiwemo zilizowashirikisha wakali kama vile rapa Kwesta, L-Tido, Kiddominant, Yanga Chief, Stogie T na wakali wengine.

Comments

comments

You may also like ...