Header

Jah Prayzah na Diamond Platnumz wapiga Debe la Upendo na ushikaji wao kwa picha

Msanii wa muziki na Staa wa wimbo ‘Watora Mari’ kutoka nchini Zimbabwe, Jah Prayzah ameweka wazi upendo na ukaribu wake kwa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Bongo Fleva.

Jah Prayzah mwenye umri wa miaka 30 ambaye jina lake kamili ni Mukudzeyi Mukombe, kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha yake akitumia Kifaa chake cha mawasiliano ‘Computer’ tayari kwa Mahojiano ya Mtandaoni kwa njia ya Skype huku nyuma yake Screen ilionesha Video ya wimbo wake ‘Angel Lo’ aliomshirikisha Jah Cure na upande wa mkono wake wa kushoto ilionekana picha kubwa ya mchoro wa rangi wa Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz.

Katika Picha hiyo ya Jah Prayzah kwenye ukurasa wake wa Instagram ilivutia wengi hasa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva na wengine ambao sura ya Diamond Platnumz sio ngeni kwao, walionesha kuiona ishara hiyo ya upendo wake kwa Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva ambapo pia Diamond Platnumz alijitokeza kuweka neno lake kwenye uwanja wa maoni. Aliandika “BROTHER FOR LIFE…”, Jah Prayzah naye alijibu “For real my G… ” na kumtag Diamond.

Post ya Jah Prayzah

 

Getting ready for my skype interview 😇 good morning fam❤️

A post shared by Jah Prayzah (@jahprayzah) on

Comments

comments

You may also like ...