Header

Star Boy ‘Wizkid’ kutumbuiza kwenye Ufunguzi wa Kombe la Dunia 2018?

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Wizkid ‘Star Boy’ ametajwa kuwa kati ya wakali watakaotoa Burudani kwenye sherehe za ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa mwaka 2018 itakazofanyika leo Juni 14, 2018, Urusi.

Wizkid ambaye jina lake kamili ni Ayodeji Ibrahim Balogun hajatoa taarifa yoyote rasmi juu ya ushiriki wake kwenye Kombe la Dunia lakini Ripoti kadhaa za mitandao nchini Nigeria zilitoa taarifa kuwa Star Boy huyo atatumbuiza pamoja na wanamuziki mwingine wa kimataifa kama vile Will Smith, Nicky Jam na Era Istrefi, ambao watakuwa wakiperform wimbo rasmi wa mahudhuhi ya michuano ya Kombe la Dunia.

Katika baadhi ya taarifa juu ya Orodha ya hao kutoa Burudani, iliripotiwa kuwa watataoa Burudani dakika 30 kabla ya mpambano wa ufunguzi katika ya Saudi Arabia and Urusi.

Comments

comments

You may also like ...