Header

Walid na Nandy wakutana jikoni, ‘watazima Moto wa Namna Gani’?

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayefanya kazi chini ya lebo ya muziki ya Amari Musiq inayomilikiwa na staa wa muziki nchini Nigeria, Patrick Okorie ‘Patoranking’, ‘Walid’ ameonekana akiwa Studio na hitmaker wa nyimbo ‘Kivuruge’ na ‘Ninogeshe’, Faustine Charles ‘Nandy’.

Nandy

Walid ambaye jina lake kamili ni Walid Ali mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa anaye fanya vizuri na kolabo ya wimbo wake ‘Namna Gani’ aliomshirikisha Boss wake, Patoranking aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Msanii Nandy na Mtayarishaji Goncha katika studio za Wanene na kuhisiwa kuwa kuna uwezekano kukutana kwa watatu hao studio, upo uwezekano wa wao kuandaa wimbo.

Walid Ali ‘Walid’

Hata hivyo kukutana kwao studio kama Walid na Nandy watafanya wimbo na ukatoka baada ya single yake ya ‘Namna Gani’ basi Nandy atakuwa ni msanii wa kwanza wakike kushirikiana na Walid tangu atangazwe rasmi kuwa msanii chini ya Amari Musiq baada ya kuachia kolabo mbili alizomshirikisha Patoranking.

Post ya Walid

Caption jamani… @officialnandy @goncherbeatz @wanenestudios

A post shared by Walid 🇹🇿 (@walidiy) on

Comments

comments

You may also like ...