Header

‘Hatujaanzisha Chombo cha Habari ili kuharibia wengine’: Diamond Platnumz

Staa wa muziki nchini Diamond Platnumz amesema kuwa lengo lake pamoja na Uongozi wote wa WCB kuanzisha Chombo cha Habari si kwa nia ya kuwaharibia wengine bali kujaribu kuiendeleza Sanaa ya Muziki na Filamu nchini.

Diamond amezungumza hayo mbele ya Waandishi wa Habari hii leo katika Hotel ya SLIP WAY iliyopo Masaki jijini Dar es salaam wakati akizindua rasmi channel ya Wasafi Tv itakayokuwa inapatikana kwenye King’amuzi cha StarTimes Channel namba 444 ikiwa ni sehemu ya kuwapata Wapenzi wa burudani kote nchini wakati wa kufurahia Burudani.

“Aliyetangulia katangulia Tu hatuna lengo la kuwaharibia Watu wa Vyombo vya habari vingine lengo letu ni kuifanya Sanaa ifike mbali na kuwawezesha wasanii waweze kupata kipato chao kupitia Muziki wao”. Alisema Diamond aliyeongozana na Mameneja wake Mkubwa Fella na Babu Tale.

Aidha Diamond aliongezea kuwa Chaneli ya Wasafi TV kama walivyodhamiria kuleta mapinduzi katika tasnia ya burudani nchini ni dhahiri kuwa king’amuzi cha StarTimes kitasaidia kulifikia lengo hilo, hasa kupitia teknolojia yake ya urushaji wa matangazo ya kidigitali.

Kwa Upande wa StarTimes Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Ndg David Malisa aliongezea kuwa “kuanzia sasa Wasafi TV itapatikana katika ving’amuzi vyetu vya Antenna, kwa hiyo watumiaji wa Antenna wanaweza kutazama chaneli hii mpya ikiwa na vipindi vipya ambavyo vitatangazwa baadaye, Wasafi TV kwa sasa inapatikana kwenye Antenna pekee, na muda wowote kuanzia sasa itakuwa tayari kwa watumiaji wa ving’amuzi vya dish pia’.

 

 

Comments

comments

You may also like ...