Header

TECNO SPARK 2, Angaza Nyakati za Maisha yako.

TECNO inafanya vizuri sana kwenye soko la ‘smartphone’ Tanzania. Hii inajidhihirisha kutokana na jinsi simu ya Spark ilivyofanya vyema mwaka jana. Mwaka huu TECNO wamekuja na Spark 2 ambayo imeboreshwa zaidi maalum kabisa kwa ajili yako wewe.
Imekuja na umbo jembamba pia ni nyepesi yenye nchi 6.0 HD+ na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9 kwa kuweza kuona vizuri zaidi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kwenye skrini yako.

Kamera ya Spark 2 ni ‘megapixel’ 13 nyuma ikisindikizwa na flash tatu zilizokaa pamoja sehemu moja na ‘megapixel’ 8 mbele yenye flash mbili zilizokaa pamoja. Hivi vionjo vyote vinafanya kazi kwa pamoja ikiwa ni kung’aza picha na kupiga picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu.
Uwezo wa ‘Portrait mode’ umeongezwa kwenye kamera ya mbele ili pale unapopiga selfie yako, sura yako inakua inaonekana vizuri kabisa. Pia kwa mfumo wa mixed flash 2.0, mwanga wa flash ya mbele umeongezwa kwa 40% na ule wa flash ya nyuma kwa 70%.
Spark 2 ina aina mpya ya ‘security’ yenye ulinzi madhubutu ambayo ni ‘face id’. Kupitia ‘face id’ una uwezo wa kufungua simu yako haraka zaidi kwa kuitazamanisha sambamba na paji la uso. Lakini pia ina ‘fingerprint’ yenye kufungua simu yako kupitia alama za vidole.
Pamoja ya kua kifaa hiki kinaendeshwa na Android 8.1 pamoja na processor ya 1.3Ghz quad core yenye kuipa simu kasi ya kufanya kazi kwa haraka zaidi na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka, lakini bado Spark 2 ina betri lenye ujazo wa 3500mAh. Kupitia Spark 2 unapata uhuru wa kusikiliza mziki, kupiga picha na kufanya kazi mbalimbali pasipo kikomo.
Kwa wale wapenzi wa simu nzuri, hakika hiki ni kifaa kwa ajili yako.

Kwa maelezo zaidi tembelea http://bbs.tecno-mobile.com

Comments

comments

You may also like ...