Header

MTAZAMO WA WADAU KUHUSIANA NA Infinix HOT 6

Baada ya ujio wa Infinix HOT 6 na kufanya vizuri sokoni kutoka na muonekano na uwezo wake lakini pia
wadau wameweza kuongelea upande wake wa pili na kuweza kuyawasilisha kama ifuatavyo.
Infinix HOT 6 ni simu iliyoboreshwa zaidi katika vionjo vya muziki kama vile spika mbili ikiwa na maana
imemlenga zaidi mpenzi wa muziki hivyo basi tulitegemea Infinix HOT 6 kuja ikiwa na headphone kama
ilivyo kwa TECNO BOOM J8 na si vi earphone.
Na kulingana na teknolojia kuendelea kukuwa tulitegemea Infinix HOT 6 yenye kasi ya 4G lakini hapa
tumeona kampuni ya simu ya Infinix wameturudisha kwenye mfumo wa 3G tunategemea mabadiliko ya
mtandao katika matoleo yanayokuja.
Sifa nyengine ambayo ni kijivunia ni uwezo wa kamera simu inakamera nzuri sana ya megapixel 13
nyumba ikiwa na flashi mbili na megapixel 5 mbele ikiwa na flashi. Infinix HOT 6 inakupa uhakika wa
picha nzuri wakati wowote ule hata katika mwanga hafifu. Lakini pia muonekano wake unavutia sana
ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 kwa nchi 6.0.
Katika upande wa Android ipo vizuri sana Infinix HOT 6 imekuja na Android 8.1 yenye kuzuiya uishaji wa
chaji katika simu kwa haraka lakini pia imesaidia simu kuwa na ‘application’ mpya kama vile face id lakini
pia imeongeza ufanisi katika simu

.

Kuhusiana na uwezo wa processor sio kama vile tulivyotegemea tumeona simu nyingi zikija na
Qualcomm spandragon kama ilivyo kwa toleo la awali la Infinix HOT S3 lakini kampuni imeturudisha
nyuma na MTK6580 processor ya 1.3 ghz quard core.
Na uhakika wa kudumu na chaji ni mkubwa inabetri ya ujazo wa 4000mAh inaweza kuhimili matumizi
ndani ya siku mbili pasipo kuzima.

Comments

comments

You may also like ...