Header

INASEMEKANA Infinix KUSHIRIKIANA NA GOOGLE KATIKA UZINDUZI WA SIMU MPYA BARANI AFRIKA.

TANZANIA, 23/6/2018: inasemekana kampuni ya simu ya Infinix kuzindua simu mpya ikiwa ni
muendelezo wa Infinix NOTE 4 kwa kushirikiana na GOOGLE. Uzinduzi huo unategemewa
kufanyika mnamo mwezi wa sita barani Afrika nchini Dubai katika jengo la Burj Khalifa.
Kwa pamoja ikishirikiana na GOOGLE kampuni ya simu ya Infinix imeweka nia ya kuzindua simu
iliyo na ubora zaidi ya matarajio ya wengi na inasemekana kupitia ushirika wake na GOOGLE
ujio wa simu zote za NOTE kutumia mfumo wa Android 1 (A1) wenye ufanisi zaidi ya Android
Oreo.
Zaidi ya watu 200 mpaka sasa wameshapata mwaliko kutoka katika kampuni hizo mbili kwenda
kushuhudia uzinduzi huo pamoja na kushuhudia namna Android 1 (A1) inavyofanya kazi kupitia
GOOGLE Assistant na GOOGLE Lens.
Akiongelea mafanikio ya kampuni, muongeaji wa kampuni ya Infinix Bwana Erick Mkomoye
alisema kwamba, “tangu kutambulishwa kwa kampuni ya Infinix mwaka 2013, kampuni
imeweza kudhihirisha ubora wake na kuweza kupenya katika masoko ya Afrika na tuko mbioni
kuwaletea teknolojia mpya kupitia simu mpya itakayozinduliwa wiki ijayo.

Comments

comments

You may also like ...