Header

Mayweather akumbwa na Shitaka la Utapeli wa zaidi ya Milioni 700 za Kitanzania

Bondia Mstaafu Floyd Money Mayweather amefunguliwa mashataka na kampuni kutoka nchini Nigeria ya Zinni media kwa madai ya kuwa Maywether ameilaghai Kampuni hiyo.

Vyombo vya habari kutoka Marekani vinaripoti kuwa Mayweather alikubaliana na Kampuni hiyo kufanya special appearance 5 nchini Nigeria na Ghana na walikubaliana na kampuni hiyo kuwa atalipwa dollar za kimarekani 375,000 amabazo ni zaidi ya million 700 za kitanzania, na walimlipa dollar za kimarekani 210,000 ambazo ni zaidi ya million 400 za kitanzania . Floyd alitengeneza mpaka video ya kuthibitisha uwepo wake lakini hakutokea hali iliyosababishia hasara kubwa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo iliingia tena Makubaliano na Mayweather kwa mara ya pili walikubaliana tena  atakuja mwezi Desemba Mwaka jana na wakakubaliana kumlipa Dola za kimarekani 550,000 amabazo ni zaidi ya billion 1 za kitanzania lakini hakutokea tena.

Juhudi za Kampuni hiyo kuongea na Uongozi wa   Mayweather ili afidie gharama zilizopotea hazikuzaa Matunda. Kampuni hiyo imeamua kufungulia mashtaka mwanamichezo huyo na inabidi alipe dollar za kimarekani million 2 ambazo ni zaidi ya billioni 4 za kitanzania.

Comments

comments

You may also like ...