Header

Trend Solar waleta neema kwa watanzania

Kampuni ya Trend Solar, inayotoa huduma za Umeme wa kulipia usiotegemea gridi nchini Tanzania, siku ya leo imezindua programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini. Trend Solar ilianza huduma yake mwaka 2017, chini ya waasisi wake Irfan Mirza na Matt Tam ambao hubuni, kusambaza na pia hufadhili miradi ya umeme wa jua ambayo inalenga kuwafikia wakazi wenye kipato cha chini na maeneo ambayo umeme wa gridi haujafika. Katika kipindi cha majaribio Trend Solar wameweza kuuza zaidi ya seti 500 kutoka kwenye maduka yao Dar es Salaam, Geita na Bagamoyo, na sasa kampuni hiyo itaongeza vifaa zaaidi Afrika Mashariki nzima ili kulifikia soko la umeme wa jua linalokadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani Bilioni 3.1 barani Afrika.

Hii ni kampuni ya kwanza kuunganisha simu za mkononi, IoT na umeme usiotegemea gridi huku ikileta simu janja yenye 4G pamoja na vifaa vingine vya nyumbani. Kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano ya simu katika bara la Africa, Trend  Solar huwapatia wateja wake paneli za sola, na simu janja yenye 4G na kioo cha inch 5.0, pia simu inakuja na intaneti ya bure kila mwezi itakayoifanya simu hiyo hiyo kutumika kama modemu na kugawa internet kwa jamii hizo. Kwa sasa kampuni ya Trend Solar ina mawakala 30 ambao huzungukia maeneo mbalimbali kutoa elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vyake.

Akizungumza katika uzinduzi, mwanzilishi na CEO wa Trend Solar Bw. Irfan Mirza alisema “Kupitia Trend Solar tunawaondolea watu wetu tatizo la kusahaulika kwenye maendeleo ya kidigitali kwa kuwapatia simu ya gharama nafuu + intaneti ya bure + na vifaa vya kuchajia nyumbani. Tunaboresha zaidi biashara ya upatikanaji wa umeme mbadala na intaneti kwa kuwa kampuni ya kwanza duniani kuunganisha Simu na mfumo wa solar za majumbani (SHS).

“Katika kipindi cha majaribio tumepokea mrejesho mzuri zaidi ya tulivyotegemea na hasa baada ya kuongeza Simu janja yetu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa watumiaji, ambao hawakuwa na njia ya kupata intaneti hapo awali. Sasa tuko katika nafasi nzuri ya kuwafikia watu milioni 36 ambao hawapati umeme wa gridi nchini Tanzania na kuwapa fursa zaidi kunufaika na maendeleo ya kidigitali”. Aliongeza Bw. Irfan.

Uzinduzi huo umefanyika Alhamis Julai 5, 2018 na kuhudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Crooke. Kampuni hiyo pia ilitangaza kuingia mkataba wa Maudhui na Kampuni ya StarTimes ambao ndio mtoa huduma wa matangazo ya kidigitali mwenye watumiaji wengi zaidi barani Afrika ikiwa na watumiaji zaidi ya Milioni 10. StarTimes watakuwa wakitoa maudhui kwa watumiaji wa Trend Solar kupitia luninga za kidigitali na StarTimes App kwenye simu janja.

Naye CEO wa StarTimes, Ndg Walker Wang alisema, “Kushirikiana na Trend Solar ni hatua ya msingi sana kwani StarTimes tutawafikia watu wengi walioko vijijini hasa wale ambao hawapati umeme wa gridi. Tunayo furaha kubwa kushirikiana na timu hii katika mradi huu mkubwa wa luninga za kidigitali ili kuwapatia fursa watanzania wengi  zaidi kufurahia maudhui na vipindi vyetu wakiwa na familia zao”.

Mfumo wa Trend Solar wa SHS ni mahususi kwa ajili ya kuzalisha nishati safi zaidi ambayo ni mbadala kwa watumiaji ambao hawapati umeme wa gridi. Kila seti ya Trend Solar TR140 inakuwa na TV ya kidigitali ya inch 24, betri, mfumo wa kulinda betri, taa za LED, taa ya LED inayoweza kubebeka na simu janja yenye kioo cha inch 5.0 na uwezo wa 4G. Wateja wanatakiwa kulipia Tsh 90,000/= kwa malipo ya awali huku kiasi kilichobaki kikilipwa kwa awamu ndani ya miezi 12 hadi 18. Pia wateja wanaweza kuufanya maipo ya Trend Solar kupitia Mpesa, Airtel Money, Tigo Pesa na HaloPesa ambayo ni mitandao yenye mifumo mikubwa zaidi ya malipo Afrika Mashariki.

Comments

comments

You may also like ...