Header

Bahati azindua kipindi cha Tv cha Ukweli wa Maisha yake

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Bahati amefanya uzinduzi wa kipindi cha runinga chenye maudhui ya ukweli ya maisha yake kwa ujumla kwa jina ‘Being Bahati’ kitakachokuwa kikiruka kupitia Runinga ya NTV Kenya kuanzia Julai 22 Mwaka huu .

Uzinduzi wa kipindi hicho ulifanyika siku ya jana ‘Clarence House Hotel’ mjini Nairobi na kuhudhuria na Mastaa tofauti kutoka nchini humo ambapo Bahati aliongozana na wasanii kutoka kwenye lebo yake ya EMB Records, Mr Seed na David Wonder.

Akizungumza na Dizzim Online mmoja wa wasanii kutoka lebo hiyo, Mr. Seed amesema kuwa naye atakuwa sehemu ya kipindi hicho cha Tv kwakuwa yuko katika maisha ya kushirikiana kikazi na msanii Bahati.

Comments

comments

You may also like ...