Header

Barack Obama ashauri vyombo vya Habari kutumika zaidi kutangaza Utalii wa Tanzania

Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Hussein Obama ‘Barack Obama’ Amesema kuwa Taifa la Tanzania lina vivutio vingi vya kitalii na njia rahisi ya kutangaza vivutio hivyo ni kuweka nguvu zaidi kwenye vyombo vya habari jambo litakalo changia kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa nchi.

Barack Obama amekuwa na Ziara ya siku nane ya mapumziko kimya kimya nchini Tanzaniana aliwasilia Jumapili ya Julai 8 ambapo aliongozana na familia yake na katika mapumziko yao walifanya matembezi kwenye hifadhi ya taifa ya Serengeti. Baada ya kuhitimisha ziara hiyo nchini Tanzania, aliekea nchini Kenya kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa kituo kimoja cha hisani eneo alikozaliwa babake Kogelo, Siaya magharibi mwa Kenya.

Hata hivyo Barack Obama ameonesha kuvutiwa na taifa la Tanzania hata kuahidi kuwa angependa kurudi tena kwa matembezi na atawashiwishi watu wake wa karibu nao kufanya matembezi nchini Tanzania ili wafurahie vivutio vinavyopatikana nchini humu.

Rais huyo Mstaafu bi Mara yake ya pili kuja nchini, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Julai 2013, wakati ambao alikuwa bado yuko madarakani. na ziara yake ilikuwa ya kikazi Ziara yake hiyo ya kikazi na ilikuwa ni sehemu ya kukamilisha ratiba yake ya mwisho ya ziara barani Afrika wakati akiwa Rais.

Comments

comments

You may also like ...