Header

Mtayarishaji Magix Enga atangaza kimya cha mwaka, kurudi tena mwaka 2019

Mtayarishaji na msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Magix Enga ametangaza kupumzika utayarishaji wa muziki na kudai kuwa ataonekana tena katika tasnia hiyo mwakani(2019).

Magix kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka ujumbe wenye kuthibitisha kuwa ameamua kupumzika utayarishaji wa muziki kwa muda na kutoa sababu kuwa atakuwa akipata kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi juu ya muziki na utayarishaji kwa ujumla.

Post yake kwenye Ukurasa wake.

Magix mbali na kufanya vizuri na nyimbo zake mwenye kama Msanii, ametayarisha hit single kadhaa zikiwemo Kasayole ya Rapa Khaligraph Jones ft Timmy T Dat, Wembe ya Timmy T Dat ft. Otile, Here we ya Prezzo ft. Gabu wa Punit & Kristoff na nyinginezo nyingi.

Hata hivyo Mtayarishaji Magix Enga kwa sasa anafanya vizuri na nyimbo zake kadhaa, Miogoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na Shida aliyomshirikisha Khaligraph Jones, Love You ft. NaiBoi, Some Love na nyingine nyingi ambazo asilimia kubwa ametayarisha mwenyewe.

Comments

comments

You may also like ...