Header

Falz asimulia kunusurika kifo kilichochukua Uhai wa Dereva wa gari lao

Rapa na Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Folarin Falana a.k.a Falz The Bahd Guy amesimulia kwa namna alivyonusurika kifo kwenye ajali mbaya ya gari kilichochukua uhai wa dereva wa gari lao  aliyepigwa risasi.

Staa huyo na mkali wa wimbo ‘La Fête’ alisimulia tukio hilo lililomtokea Mwezi Novemba mwaka 2013 ambapo alieleza kuwa ilikuwa ni ki[indi chake alichopata malipo ya cheque ya Naira Milioni Moja baada ya kutoa Burudani katika sherehe ya harusi. Malipo hayo kwa Falz akiyataja kuwa ni malipo makubwa kwake kwa mara ya kwanza kulipwa katika muziki wake.

Falz aliendelea kusimulia kuwa, akiwa na marafiki zake baada ya show yake hiyo aliyopata malipo mazuri mjini Abuja, walipanga safari kwenda mji wa Benin akiwa na marafiki zake na walikubaliana kutumia usafiri wa gari.

Njiani walitokewa na tukio lililopelekea gari lao kuyumba na gari lao hilo uliposikika mlio mkubwa wa ghafla na baada ya gari kupata ajali walivamiwa na watu waliohisiwa kuwa ni majambazi. Watu hao ndio waliosababisha ajali baada ya kumpiga risasi dereva wao na kuwavamia wakiwataka wawape pesa.

Wakiwa katika hali ya kutojielewa na wasijue nini kilitokea na kinachoendelea wakati huo walipata msaada kutoka kwa wasamalia wema ambapo walipelekwa hospitalini kwa matibabu.
Chanzo: Concise News.

Comments

comments

You may also like ...