Header

NEW VIDEO: LEVEL -BEKA THE BOY X PETRA!

Msanii Beka the Boy

 

Wakati ushindani mkuu unao shuhudiwa nchini Kenya kimuziki unavyozidi kuwaka moto, wasanii wakuimba haswa wanao tokea upande wa Pwani ya Kenya wamekuwa wakiumiza vichwa haswa huku kila mmoja akija na mawazo yake kivyake ilimradi kuwabwaga wenzake. Kuna wasanii wanao tumia kiki za mahusiano yao ya kimapenzi ili kulikwaruza nakuliteka soko la muziki nchini Kenya kama mfano uliohai akiwa ni Otile Brown ambaye amefanikiwa kuliteka soko la muziki kupitia mahusiano yake na mrembo Vera Sidika na kunao wanao tumia Camera za hali ya juu kutengeneza ubora wa video kali zenye hadhi ya kimataifa kama msanii Beka the Boy ambaye ndiye gumzo zaidi kwasasa nchini Kenya kwa jinsi anaovyotoa vibao vyake kila mara, yani kwamwezi mara mbili huku ubora wa video zake zote ukiwa wa hali ya juu kitu ambacho kimeanza kuwashangaza na kuwavutia wadau wengi zaidi.

Beka the Boy akiwa na rapper wakike Petra

Beka the Boy akiongea na meza yetu ya habari kuhusu wanao kosoa hulka yake ya kutoa vibao vya muziki kila mara na video kali zenye kupitiliza viwango vya waastani, amejibu swala hili kwa kunadi kuwa yeye hufunya hivyo kwa kuwaridhisha mashabiki wake wapate mkusanyiko na vionjo tofautitofauti za sanaa yake mwenye. Beka anakuwa msanii tajika miongoni mwa wasanii wanao tamba kwasasa nchini Kenya na hii inatokana na bidii yake anayoiweka kwenye tasinia ya muziki. Anaamini kuwa msanii anayekuwa na kipaji alichojaliwa na Mungu tangia kuzaliwa huwa haaishi mawazo kama wale wasanii wano charibu kulazimisha mambo kwenye sanaa haswa ya muziki kwa kuukurupukia umaarufu. Kitu ambacho kina mfanya kuwa na msukumo na ari ya kutoa kazi nzuri na za kuvutia kwa mpigo kila mara.

Picha| Behind the scene ya video ya Level| courtesy Dizzimoline

Video hii hapa chini ya wimbo huu kwa jina level, uliotoka mwanzoni mapema mwezi huu, video hii ilifanyiwa jijini Nairobi Kenya huku ikiwa ndio video yake ya kwanza kumshirikisha rapper mkali na wakike kutoka Kenya kwa jina Petra na mkaazi wa Nairobi. Tayari kupitia channel yake ya YouTube ukanda huo wa video ya Level unazidi kuwavutia watu wengi kwa jinsi ulivyotayrishwa kwa mbinu za juu zaidi na kisasa kitu ambacho kinamfanya Beka the Boy kuwa tishio kwa wasanii wakubwa wa kuimba nchini Kenya wakiwemo wasanii kama Otile Brown na kundi kubwa la muziki Barani Afrika kutoka Kenya Sauti sol na wengine wengi. Nimekusogozea kibao chenyewe hapa chini ili uweze kukitazama. Burudika!

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...