Header

Redsan awashirikisha Patoranking, Demarco, Nayla na wengine kwenye Album yake mpya ‘Baddest’

Msanii wa muziki wa Danso kutoka nchini Kenya, Redsan ametangaza tarehe rasmi ya kuachia Album yake Mpya itakayokwenda kwa jina ‘Baddest’.

Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Swabri Mohammed, aliweka ujumbe wa kutangaza kuwa tarehe 1 mwezi Septemba mwaka huu ataachia Album na kuweka Hashtag mbili tofauti ambazo ni #baddest na #king.

September 1st.. #king #baddest

A post shared by 👑👑R.E.D.S.A.N (@redsanmusic) on

 

Kwa Mujibu wa Chanzo cha kuaminika, imebainika kuwa album hiyo ya Redsan itabeba nyimbo zipatazo 12 na kati ya mastaa walioshirikishwa ni pamoja na Patoranking kutoka Nigeria, Demarco na Mwimbaji Nyla wa kundi la Brick & Lace kutoka nchini Jamaika, Avid kutoka Tanzania, na wengine kibao.

Hata hivyo watayarishaji ambao tayari wameshashiriki katika kuandaa nyimbo kadhaa zitakazopatikana katika album hiyo ni pamoja na Producer Sappy Chini ya Sappy Music Lab ambaye amesimamia asilimia kubwa ya utayarishaji, Jilly Baby kutoka nchini Kenya na Fahrenheitz kutoka nchini Angola.

Redsan na Producer Sappy ndani ya Studio za Sappy Music Lab

 

Comments

comments

You may also like ...