Header

Jua Cali aachia wimbo kutoka kwenye Album ambayo Joh Makini ni kati ya walioshirikishwa

Mkongwe na Staa wa muziki wa Genge kutoka nchini Kenya, Paul Julius Nunda a.k.a Jua Cali ameachia video ya wimbo wake kwa jina ‘Najitoa’ na video ya wimbo huo imengozwa na Director Thomeski.

Kikubwa ambacho hakikutegemewa ni video ya wimbo huo kuandaliwa na kuonekana katika muonekano wa vibonzo/Animation chini ya ufundi wa Wambaa Muiru.

‘Najitoa’ ni wambo wa nne wa Jua Cali kutoka kwenye Album yake inayotarajiwa kutoka kwa jina la ‘Mali ya Umma’.

Hata hivyo kipindi cha nyuma Jua Cali alishamtaja Joh Makini kuwa ni kati ya mastaa wa muziki wa rap kutoka Tanzania watakao shirikishwa katika album hiyo.

Itazame video ya wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...