Header

Tekashi 6ix9ine Akanusha taarifa za kuvamiwa kwake na Kiki ya Kolabo ya wimbo wake na Nicki Minaj

Rapa Mmarekani, Daniel Hernandez ‘Tekashi 6ix9ine’ ameelezea kilichotokea wakati wa kushambuliwa kwake Jumapili ya wikiendi iliyopita, ambapo alidai kuwa alitekwa kwa kuwekewa bastola, alipigwa vibaya kisha kuibiwa vitu vya thamani ya $ 750,000 na fedha taslimu zaidi ya $ 15,000.

Tekashi katika moja ya mahojiano ya karibuni alisimulia kuwa alikuwa akirudi nyumbani baada ya kuhariri video yake ya “FEFE” aliyomshirikisha Nicki Minaj ambapo gari lake liligongwa kwa nyuma.

Muda mfupi watu wasiojulikana walitoka kwenye gari wakiwa na bastola na kuanza kumshambulia amnbapo alipoteza fahamu na muda uliofuata alijikuta kwenye gari tofauti.

Rapa huyo alikanusha taarifa za waliohusisha tukio hilo la uvamizi kuwa ilikuwa ni njia ya kutafuta attention ingwa alikiri kuwahi kufanya hivyo siku za nyuma.

Comments

comments

You may also like ...