Header

Watanzania wasogezewa Burudani ya Michuano ya ICC

Katika kipindi hiki cha tetesi za usajili na usajili wa wachezaji katika ligi kubwa za Ulaya huku timu nyingi zikihaha kupata aini za Wachezaji kwa ajili ya kujiandaa na Msimu ujao Vilabu mbalimbali vikubwa kutoka Barani Ulaya vinashiriki Mashindano ya ICC ambayo yanafahamika kama Mashindano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambayo hii Leo kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza kuonyesha Mashindano hayo.

Mechi hizo ambazo zimeanza kutimua vumbi wikiendi iliyopita zinashirikisha vilabu bora 18 kutoka ligi tano kubwa barani ulaya. Miongoni mwa timu hizo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund (Bundesliga), Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal (Premier League), PSG (League 1), Barcelona, Real Madrid (La Liga), AC Milan, Inter Milan na Juventus (Serie A). Katika mechi zilizopigwa wikiendi iliyopita Borussia Dortmund wameonyesha kiwango kizuri baada ya kuwafunga Manchester City 1-0 na kuwachapa Liverpool 3-1.

Hamu kubwa ya Mashabiki katika Mashindano haya ni kuona Nyota waiosajiliwa na Vilabu vyao jinsi wanavyoonyesha Viwango na kujituma kuelekea Msimu ujao ambao kwa Ligi mbalimbali Barani Ulaya zinatarajia kuanza Mwezi Ujao.

Wapenzi wa Soka nchini watapata nafasi ya kuishuhudia michuano hii kupitia chaneli ya World Football na Sports Premium katika king’amuzi cha StarTimes ambao wana haki za kuonyesha michuano hii.

 

 

Comments

comments

You may also like ...