Header

Ben Pol athibitisha kujongea kwenye kolabo na Mastaa hawa kutoka Kenya

Msanii wa muziki kutoka Tanzania na Staa wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Benard Michael Paul Mnyang’anga a.k.a Ben Pol ametfichua orodha ya baadhi ya Mastaa wa muziki kutoka nchini Kenya walioko kwenye mpango wa kufanya naye kazi.

Akizungumza na kituo kikubwa cha habari nchini Kenya katika moja ya mahojiano ya hivi karibuni, Ben Pol aliwataja Naiboi na wanakikundi cha muziki cha Elani kuwa ni kati ya Mastaa kutoka nchini humo walioko katika mazungumzo ya kushirikina naye katika kazi za muziki.

Naiboi

Hata hivyo Ben Pol ameshashirikiana na wasanii kadhaa kutoka nchini Kenya ambao ni Willy Paul, Otile Brown na Dj Creme De La Creme. Katika mahojiano hayo pia Ben litangaza kuwa ameweka mlango wazi wa kushirikiana na wasanii wengine zaidi ya hao kutoka nchini humo.

Comments

comments

You may also like ...