Header

Diamond Platnumz akalia kiti cha Usher Raymond kwenye video ya Mr. Flavour

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameonekana kukalia kiti anachokipenda kwenye video ya wimbo mpya ‘Time to Party’ alioshirikishwa na mkali kutoka Nigeria, Mr. Flavour chini ya Director Patrick Elis.

Diamond aliyewahi kubayanisha kupenda hatua za muziki na kufata nyayo za Mkali na mongwe wa muziki kutoka Marekani, Usher Raymond IV’Usher’ ameonekana kwenye video ya kolabo hiyo na Mr. Flavour katika moja scene yenye mfanano na scene aliyowahi kuonekana Usher kwenye kolabo ya wimbo wa Chris Brown, ‘New Flame’.

New Flame ya Chris Brown

Picha kutoka kwenye kipande cha Usher kutoka kwenye Video ya ‘new Flame’

 

Alivyotokea Diamond Platnumz kwenye video ya ‘Time To Party’ ya Mr Flavour.

Hata hivyo kwenye video ‘Time To Party’ kuna baadhi ya mionekanao yenye kiasi cha chembe chembe za kufanana na baadhi ya mionekano ilioonekana kwenye video hiyo ya Chris Brown, ft Usher & Rick Ross.

Comments

comments

You may also like ...