Header

Rapa kutoka Nigeria aichagua Kenya kuutangaza Muziki wake Afrika Mashariki

Msanii wa muziki na mkali wa Rap kutoka nchini Nigeria, Obigho chini ya kampuni yake Great Obigho Nation Entertainment a.k.a (GONE) ameichagua Kenya kwa Afrika Mashariki kuwa nchi ya yeye kuachia video ya wimbo wake mpya utakao kwenda kwa jina ‘Fresh’ aliomshirikisha Dj Royal.

Akizungumza na mmoja ya watayarishaji wa muziki wa nchini Kenya, Obigho amedai kuwa nje ya Nigeria kiwanda cha muziki ukanda wa Afrika Mashariki kimechanamka zaidi na soko la muziki linahitaji changamoto ya namna hiyo inayochangia kukuza kwa haraka kiwanda hicho kibiashara.

Rapa Obigho sokoni kwa sasa anafanya vizuri na nyimbo zake kama vile, ‘Switch Side’, ni wimbo mwingine ambao yuko mbioni kuuachia rasmi akiwa nchini Kenya kabla ya kurudi nchini Nigeria.

Comments

comments

You may also like ...