Header

Timbulo apiga Teke jina la Director wa video ya wimbo wake Mpya ‘Sangoma’

Msanii wa muziki na Staa wa wimbo ‘Mfuasi’, Said Timbulo ‘Timbulo’ amekwepa kutoa sababu za kwanini jina la Director halijaandikwa kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Sangoma’.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Timbulo amesema angependa ibaki hivyo kama inavyoonekana kwakuwa sio muda wa kutoa maelezo ya kina juu ya hilo, kikubwa mashabiki waendelee kufurahia uzuri wa kilichoandaliwa kwa Ujumla kuanzia audio ya mpaka video ya wimbo wake huo.

“Mimi nadhani muda huu sio wakumzungumzia Director wa video yangu, nimeandaa kazi nzuri kwa Shabiki tu. Kikubwa naomba mashabiki watoe support tu lakini hayo mengine ya Director mara yuko wapi, mara hajaandikwa…Kwa shabiki mwenye nia ya kunisupport siamini kama hasipomjua Director wa Video yangu kutafanya kazi yangu ionekana Mbaya” Alisema Timbulo.

Comments

comments

You may also like ...