Header

Young Dee amrushia Dongo Bill Nass “bora uzikwe tu tena Congo”

Msanii wa muziki wa Rap, Young Dee ‘Paka Rapa’ amemchana Rapa Bill Nass kwa jinsi alivyojitokeza katika picha aliyofananisha mavazi na kila kitu alichobeba katika Picha hiyo.

Bill Nass aliweka picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa ndani ya utanashavi wa mavazi yenye rangi na mapambo ya rangi nyekundu kwa asilimia kubwa picha ambayo Ypung Dee aliponda kwa amneno ya kisanaa yenye kuendana na wimbo mpya wa Bill Nass ‘Labda’.

Young Dee alipost picha na Kundika “Pale unaingia duka la nguo ila unaona bado unaingia na la vyombo ili umatchishe kabisa😆 @billnass !”.

Comments

comments

You may also like ...